Friday, 30 September 2016

Taarifa Ya Kanusho Kuhusu Tangazo La Ajira Serikalini

Kuna tangazo ambalo linasambazwa kupitia baadhi ya mitandao ya kijamii lenye kichwa cha habari ‘’Sekretarieti ya Ajira yatangaza zaidi ya nafasi za kazi 1,000’’. Likionyesha kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia watanzania wenye sifa na uwezo kujaza jumla ya nafasi wazi za kazi 1,101 kwa niaba ya waajiri mbalimbali Serikalini.

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira anapenda kuwataafu wadau na wananchi wote kwa ujumla kuwa taarifa hiyo haina ukweli wowote na inalenga kuupotosha Umma, hivyo wananchi wote wanapaswa kuzipuuza. 

Matangazo yote ambayo hutolewa na Serikali kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni lazima yaonekane kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajirawww.ajira.go.tz au portal ya Ajira ambayo ni portal.ajira.go.tz.

Kama mnavyofahamu hivi karibuni Serikali ilitoa taarifa ya kusitisha Ajira mpya Serikalini kwa ajili ya zoezi la uhakiki wa Watumishi hewa kama ambavyo taarifa ilivyotolewa hapo awali, kwa kuwa zoezi hilo bado halijakamilika tunaomba wananchi wote na wadau wa Sekretarieti ya Ajira waendelee kuvuta subira hadi pale zoezi hilo litakapokamilika na taarifa rasmi itatolewa na Mamlaka husika.

Sekretarieti ya Ajira inapenda kuomba radhi kwa wale wote waliopata usumbufu kutokana na tangazo hilo lenye nia ya kupotosha Umma. 

Aidha,tunaendelea kuwasisitiza wadau wetu wote kuwa, wanapoona matangazo ya kazi yanayodaiwa kutolewa na Sekretarieti ya Ajira katika baadhi ya mitandao ya kijamii wasiyokuwa na uhakika nayo wajiridhishe kwa kuangalia katika tovuti na portal ya Sekretarieti ya Ajira kabla ya kuyafanyia kazi.

Aidha, Sekretarieti ya Ajira inapenda kutoa taarifa kuwa haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote wenye nia ya kuupotosha umma kupitia taarifa zinazosambazwa ambazo hazina ukweli.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

Tarehe 30 Septemba, 2016

Chadema Waahirisha Tena Maandamano ya Oparesheni UKUTA



Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe ametangaza kuwa Operesheni UKUTA iliyokuwa ifanyike Oktoba Mosi haitofanyika tena.

Mbowe amesema hayo leo baada ya kimya cha muda mrefu tangu kuahirishwa kwa maandamano Septemba Mosi. Aidha, Mbowe amesema kuwa hawatataja tarehe ya kufanya maandamano ili kutompa adui nafasi ya kujipanga. Amesisitiza kuwa maandamano yapo, ila tarehe hawataweka hadharani.

Operesheni hii ilikuwa ifanyike Septemba Mosi mwaka huu lakini iliahirishwa ili kuwapa nafasi viongozi wa dini kuweza kukutana na kujadiliana na Rais Dkt Magufuli juu ya mustakabali wa hali ya kisiasa nchini kufuatia kuzuiwa kwa shughuli mbalimbali za kisiasa.

Hadi leo viongozi wa dini bado hawajakutana na Rais Magufuli licha ya wao kueleza kuwa Rais Magufuli hajakataa kukutana nao kama inavyoelezwa na baadhi ya vyombo vya habari

Waziri mkuu kuhamia rasmi dodoma leo

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, anatarajia  kuhamia rasmi Dodoma leo. 

Majaliwa anahamia mjini hapa ikiwa ni sehemu ya kutekeleza ahadi ya Serikali ya awamu ya tano ya kuhamia Dodoma ambako ndiko yaliko makao makuu ya nchi. 

Julai 25 mwaka huu, katika kilele cha siku ya mashujaa kilichofanyika mkoani hapa, Waziri Mkuu Majaliwa alisema ifikapo Septemba mwaka huu, Serikali itakuwa imehamia mjini hapa. 

Hatua hiyo ya  waziri mkuu   ilitangazwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alipozungumza  na waandishi wa habari. 

Alisema   Waziri Mkuu anatarajiwa kuwasili leo mchana akitokea   Dar es Salaam alikokuwa akiishi. 

“Baada ya kuwasili hapa  atafanya ziara ya siku mbili katika Manispaa ya Dodoma Oktoba mosi na Oktoba 2 mwaka huu   kukagua hatua mbalimbali za maandalizi ya kupokea   Serikali mkoani hapa. 

“Wakati wa ziara hiyo, atakagua majengo ya Serikali, maeneo ya kutolea huduma za afya, kituo cha umeme cha Zuzu, masoko, chanzo cha maji Mzakwe na maeneo ya viwanda. 

“Kwa hiyo  maandalizi yote muhimu kwa ajili ya mapokezi ya waziri mkuu yamekamilika na uongozi wa mkoa unaendelea kuwajulisha wananchi na wadau wote katika maeneo yatakayohusika na ziara hiyo, washiriki kwa ukamilifu. 

“Kwa niaba ya uongozi wa Mkoa wa Dodoma, tunampongeza Waziri Mkuu Majaliwa kwa kuitikia na kutekeleza uamuzi wa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa kuhamia makao makuu mjini hapa,”

TAARIFA KUHUSU KESI YA VIONGOZI WALIOFUNGUA AKAUNTI BANDIA YA MAAFA KAGERA.

Watumishi  watatu wa Serikali akiwamo Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Bukoba, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba wakituhumiwa kutaka kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu.

Watumishi hao wanadaiwa kutaka kujipatia fedha hizo baada ya kufungua akaunti feki iitwayo kamati ya maafa Kagera kwa ajili ya kukusanya fedha za kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Septemba 10 mwaka huu.

Watumishi waliofikishwa mahakamani hapo jana ni aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Amantus Msole, Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Kelvin Makonda, Mhasibu wa Mkoa wa Kagera, Simbaufoo Swai na Meneja wa CRDB tawi la Bukoba, Carlo Sendwa.

Akisoma mashtaka hayo, Wakili wa Serikali, Hashimu Ngole, alidai watuhumiwa hao wanashtakiwa kwa makosa mawili.

Alilitaja shtaka la kwanza kuwa ni kula njama za kutenda kosa la kufungua akaunti feki yenye jina linalofanana na jina la akaunti iliyofunguliwa na Serikali kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi.

Aliitaja akaunti hiyo kuwa ni yenye jina la Kamati Maafa Kagera yenye namba 015225617300.

Kwa mujibu wa wakili huyo, watuhumiwa hao badala ya kutumia akaunti ya Serikali kukusanya fedha za maafa, walifungua akaunti yao waliyoipa jina la Kamati Maafa Kagera yenye namba 0150225617300.

Alilitaja shtaka la pili kuwa ni watuhumiwa kutumia madaraka na vyeo vyao vibaya kinyume cha sheria.

Mawakili wanaowatetea watuhumiwa hao walimwomba hakimu awapatie dhamana wateja wao kwa kuwa bado ni watumishi wa Serikali na wanao uwezo wa kujidhamini wenyewe na hawawezi kutoka nje ya Kagera.

Washtakiwa hao walirejeshwa rumande ambapo kesi hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo Septemba 30 na hakimu atatoa maamuzi kuhusu dhamana yao.

Hatimae Man United wapata ushindi wa kwanza Europa League

Baada ya kuanza vibaya kwa klabu ya Man United katika mchezo wake wa kwanza wa Europa League dhidi ya Feyenoord nchini Uholanzi, usiku wa Septemba 29 Man United walishuka tena dimbani kucheza mchezo wao wa pili wa Kundi A Europa League dhidi ya Zorya.Man United ambao mchezo wa kwanza walipoteza kwa goli 1-0 dhidi ya Feyenoord ambao walikuwa na rekodi ya kushinda mechi nane mfululizo, wamecheza mchezo wao wa pili wa Europa League dhidi ya Zorya katika uwanja wao wa Old Trafford na kufanikiwa kushinda kwa goli 1-0 lililofungwa na Zlatan Ibrahimovic dakika ya 69.

Thursday, 29 September 2016

Scan vyeti vyako kwa simu, download camscanner application hapa

Camscanner ni application nzuri yakuscani
Vyeti, au kitu chochote kilichopo kwenye hardcopy na kuviweka katika softcopy. Hakuna haja ya kwenda stationary
https://www.camscanner.com/mobile/faq?language=en-us&platform=android&device=phone&vendor=Market&version=4.0.1.20160728&type=download_and_purchase



 Download hapa application yakuscani Vyeti https://www.camscanner.com 
Jinsi yakuitumia.
 a)  Fungua application yako ya camscanner
b) utaona icon ya camera bonyeza hapo
c) piga picha Cheti chako na utaweka size unayotaka wewe(crop) 
d) save scanned material in PDF form, unaweza kutuma kwa email na mtu akakiprint kama kawaida

Mpina ataka wanaosoma 'cheti' nao wapewe mikopo

Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira Luhaga Mpina amesema umefika wakati wa bodi ya mikopo ya elimu ya juu kuangalia upya sera ya ukopeshaji ili waweze kutoka mikopo kwa ngazi ya Astashada kwa masomo ya Sayansi ili kupata wataalam wengi wa fani hiyo
 
Mhe. Mpina amesema kuwa hatua hiyo itawezesha kwenda sambamba ma mapinduzi ya maendeleo ya uchumi wa viwanda jambo ambalo litawezesha taifa kuwa na wataalam wengi wa mambo ya Sayansi na kuongeza tija katika ustawi wa maendeleo ya viwanda.

Akiongea na uongozi wa juu wa bodi ya mikopo ya elimu ya Visiwani Zanzibar, amesema Tanzania sasa inataka kuingia katika uchumi wa viwanda jambo ambalo linahitaji wataalam wengi wa masomo ya Sayansi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo Tanzania, Abdul-Razaq Bandru, amesema kuwa bodi hiyo inafanya marekebisho mbalimbali ikiwemo kufanikisha mabadiliko ya kanzidata ili kuwafikia wadaiwa kwa urahisi zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Luhaga ametoa pongezi kwa tume ya taifa ya nguvu za atomic visiwani Zanzibar na kuwambia kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kuimarisha na kuisimamia ofisi za tume hiyo visiwani Zanzibar.

MIX PICHA 10: Ndege inayotajwa kwa ubora na yenye starehe kuliko zote duniani

Mtu wangu wa nguvu leo nimeipata hii ya Ndege inayotajwa kuwa na starehe za kutosha ikiwa imetengenezwa ubora kuliko Ndege yoyote ile duniani. Ndege hii inafahamika kama “World’s Most Luxurious Commercial Jet ikiwa na jina la kibiashara Crystal.



Crystal Plane ina mgahawa wa kisasa zaidi kuliko hata migahawa ya mitaani, Bar ambayo ni Classic sana, pamoja na huduma ya Internet yenye kasi zaidi ya Wi-Fi… Ndege hii inamilikiwa na kampuni kutoka nchini Marekani.

Gharama za kuikodi ndege hii ni dola za Marekani elfu hamsini kwa siku moja huku abiria akipewa huduma ya hadhi ya hoteli ya five star. Ndege hii inatarajiwa kuanza kutumika na wateja ifikapo mwaka 2017.

Nimekusogezea hapa picha za ndani ya ndege hiyo mtu wangu.









Heka heka la soudy brown na Elizabeth Michael ama LuLu