Saturday, 29 October 2016

Breaking news:BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU TANZANIA IMETANGAZA RASMI KWA WANAFUNZI WOTE WALIOOMBA MKOPO KUANGALIA SASA MIKOPO WALIYOPANGIWA 2016/2017

Image result for OLAS.GO.TZ
Bodi ya mikopo ya elimu ya juu Inawatangazia waombaji wote wa mwaka wa masomo 2016/2017 ,kuangalia mikopo waliyopangiwa.
Kindly Click here to view your Loan allocation status. Please note that you will be required to use the four index number you used during your application.

Sunday, 23 October 2016

MPYA:HII HAPA LIST YA VYUO VILIVYOTOA MAJINA YA WANUFAIKA WA MKOPO 2016/2017-BATCH 1 & 2

Habari yako,kama kawaida yetu huwa tunapenda sana kuwapa kitu roho inapenda wadau wetu wakubwa ambae wewe hapo unaesoma habari hii ni mmojawapo.

Nimeamua kukuwekea hapo chini list ya vyuo ambavyohadi sasa vimetoa majina ya wanafunzi waliopata mkopo batch 1.



KWA CHUO CHA KCMC             <<BONYEZA HAPA>>
KWA CHUO CHA MAJI DSM       <<BONYEZA HAPA>>
KWA CHUO KIKUU UDSM          <<BONYEZA HAPA>>
KWA CHUO KIKUU DUCE           <<BONYEZA HAPA>>
KWA CHUO KIKUU MUCE          <<BONYEZA HAPA>>
 KWA CHUO KIKUU SUA               <<BONYEZA HAPA>> 
KWA CHUO KIKUU MUHAS        <<BONYEZA HAPA>>

Tuesday, 18 October 2016

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI MWAKA WA KWANZA WALIOPANGIWA VYUMBA CHUO KIKUU MUHIMBILI 2016/2017

MUHIMBILI UNIVERSITY OF HEALTH AND ALLIED SCIENCES

Rooms Allocations at MUHAS Hostels

Kindly informed that rooms have been allocated to both Undergraduate and Postgraduate Students  for Academic Year 2016/2017. For more details, download the Rooms Allocationand Important Notice Regarding Room Allocation.

majina ya wanafunzi waliochaguliwa third selection

Nimekuwekea hapa majina wa waliochaguliwa third selection.
mjini,Tumeamua kukuwekea list ya vyuo vikuu ambavyo vimetoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa na joining instructions za  kujiunga na vyuo vikuu 2016/2017 THIRD  ROUND



CHUO KIKUU ATC ARUSHA                    (3RD ROUND)  >>BONYEZA HAPA<<

CHUO KIKUU MUST-MBEYA                   (3RD ROUND)  >>BONYEZA HAPA<<

CHUO KIKUU AMUCTA                           (3RD ROUND)  >>BONYEZA HAPA<<

CHUO KIKUU MARIAN                           (3RD ROUND)  >>BONYEZA HAPA<<

CHUO KIKUU ST.JOHN DODOMA        (3RD ROUND)  >>BONYEZA HAPA<<

CHUO KIKUU MOUNT MERU               (3RD ROUND)  >>BONYEZA HAPA<<

Thursday, 13 October 2016

Polisi Dar yaua majambazi wanne wanaodaiwa kuwaua askari wanne waliokuwa lindo Mbagala DSM mwezi Agosti, yakamata 'Panya Road' 10.

Kikosi Maalumu cha Kupambana na Ujambazi wa Kutumia Silaha cha Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kilifanikiwa kukamata watuhumiwa wanne wa ujambazi waliohusika katika mauaji ya askari polisi 4 katika benki ya CRDB iliyopo maeneo ya Mbande, Mbagala jijini Dar es Salaam.

Kamishna wa Kanda hiyo, Kamanda Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, amesema watuhumiwa hao walikamatwa wakati wa majibizano ya risasi yaliyotokea Oktoba 11, 2016 katika pori la Dondwe lililopo Chanika.

“Kikosi kilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja, baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa ni jambazi na ndiye aliyehusika katika mauaji ya askari polisi huko Mbande,” amesema.

Kamanda Sirro ameongeza kuwa “Baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika na tukio hilo akiwa na wenzie saba, alitupeleka mahala walipo wenzake, ila alikimbia, wenzie walipojua polisi wapo maeneo hayo, walianza kurusha risasi ndipo polisi nao wakaanza kurusha risasi.”

Kamanda Sirro amesema kuwa, watuhumiwa hao walizidiwa na mashambulizi ya risasi ambapo walijeruhiwa vibaya na kwamba walifariki dunia wakiwa wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Amesema askari polisi walifanikiwa kuipata bunduki ya kijeshi aina ya SMG iliyofutwa usajili ambayo watuhumiwa hao waliipora kutoka mikononi mwa polisi waliowaua mbande ikiwa na risasi 22 ndani ya magazine.

Katika tukio lingine, Kamanda Sirro amesema mnamo Oktoba 11, 2016 maeneo ya magomeni polisi wakiwa doria walifanikiwa kukamata bastola moja aina ya bereta baada ya kutelekezwa na kundi la vijana.

Pia amesema Jeshi la Polisi limekamata watuhumiwa watatu wakiwa na bomu moja la kienyeji, mapanga manne, visu viwili, na bisibisi moja.

Vilevile Jeshi la Polisi Dar es Salaam Oktoba 12, 2016 walikamata panya road zaidi ya 10 maeneo ya Mbagala.

Wednesday, 12 October 2016

Waziri awapa ahueni walimu 4 waliotoa kipigo kwa mwanafunzi Mbeya

Baada ya uamuzi wa kuwafukuza vyuo walimu wanne waliokuwa kwenye mafunzo ya vitendo katika Shule ya Sekondari ya Kutwa ya Mbeya (Mbeya Day), serikali imesema vyuo husika vinaweza kushauri adhabu mbadala iwapo vitajiridhisha kuwepo kwa mazingira tofauti na yaliyozingatiwa kwenye uamuzi wa kuwafukuza vyuo.
tanzanie_ecole_-_copie_teaser
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alisema hayo juzi alipozungumza na waandishi wa habari mkoani Mbeya alikokuwa katika ziara kwenye shule mbalimbali mkoani humo.
Profesa Ndalichako alisema uamuzi uliochukuliwa na ofisi yake ulizingatia sheria ndogo zilizotungwa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm) zinazoainisha makosa yanayoweza kumfukuzisha chuo mwanafunzi.
Hata hivyo, alisema uamuzi uliochukuliwa unaweza kutazamwa upya na vyuo husika iwapo uzito uliochukuliwa na wizara utaonekana kuwa katika mazingira na uhalisia wa tukio husika.
Walimu wanne waliokuwa kwa vitendo katika shule ya Mbeya Day walifukuzwa vyuo baada ya uamuzi wa serikali kutokana na kuhusika kumpiga mwanafunzi Sebastain Chinguku vibao, mateke na fimbo kwa ukatili Septemba 28 mwaka huu shuleni humo.
Walimu hao walibainika baada ya kipande cha video kusambazwa katika mitandao ya kijamii hivi karibuni. Waliohusika na vyuo walivyokuwa wakisoma ni Frank Msigwa (anayedaiwa kumpiga zaidi mwanafunzi makofi kichwani), John Deo na Sante Gwamaka wote wa DUCE-UDSM, na Evans Sanga wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Akijibu swali la idadi ipi ya viboko inastahili kutolewa kama adhabu kwa mwanafunzi anayekwenda kinyume na maelekezo ya shule yake, Profesa Ndalichako alisema binafsi asingependa mwanafunzi achapwe hata kiboko kimoja lakini hilo linawezekana pale wanafunzi watakapozingatia maadili.
“Adhabu yoyote kwa mwanafunzi inatolewa pale anapokuwa amekwenda kinyume na maadili ya shule yake. Kama wanafunzi wote watazingatia maadili sidhani kama kuna mwalimu atakayempiga mwanafunzi hata kiboko kimoja. Haya yote yanatokea kutokana na wanafunzi kukosa nidhamu,” alisisitiza Ndalichako
Source: Habari Leo